Fuata vidokezo hivi vya kucheza kamari kwa uwajibikaji ili kuweza kufurahia kikamilifu uchezaji wako:
- Cheza kamari kama njia ya kujifurahisha tu - kamari sio njia ya kujipatia pesa.
- Kamwe usicheze kamari na pesa ambazo huwezi kumudu kuzipoteza.
- Weka kikomo cha pesa unayotumia kucheza kamari - amua ni pesa ngapi unaweza kumudu kupoteza kwa siku / wiki / mwezi kabla ya kuanza kucheza kamari.
- Acha kucheza kamari ikiwa umepoteza kikomo ulichoweka kutumia kwa siku / kwa wiki / kwa mwezi - usiendelee kupoteza.
- Amua ni muda gani kwa siku / wiki / mwezi utatumia kucheza kamari. Usisahau burudani zako zingine - zinastahili kupata muda wako pia.
- Usicheze kamari ikiwa unahisi una msongo wa mawazo, unaumia kihisia, au hauwezi tu kuzingatia - badala yake chukua mapumziko.
- Usicheze kamari kwa ushawishi wa pombe au madawa ya kulevya.
- Tafuta msaada mara moja ikiwa umetambua una uraibu wa kucheza kamari.